FAMILIA YA JEFF MWATHI YAOMBA MAHAKAMA KUHARAKISHA KESI
Familia ya Jeff Mwathi imeomba mahakama ziendelee haraka na kwa ufanisi na kesi inayohusu kifo chake, ikieleza kuwa mchakato huo umekuwa wa kusababisha maumivu makubwa kwao.
Kupitia wakili wao, Danstan Omari, familia imebainisha kuwa Mwathi alizikwa mara mbili, jambo lililozidisha huzuni yao na kuendelea kuendeleza maumivu ya kifamilia.
Familia imetaja kuwa wako tayari kujitokeza mahakamani wakati wowote kuhakikisha kesi inasikilizwa na kufikiwa uamuzi bila ucheleweshaji wakitafuta haki na amani ya moyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































