KAKAMEGA HOMEBOYZ YAOMBOLEZA MLINZI SILAS ABUNGANA
Kakamega Homeboyz FC na familia ya soka nchini Kenya wamegubikwa na mshtuko kufuatia kifo cha ghafla cha mlinzi wao, Silas Abungana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliyekuwa amejiunga na klabu hiyo kutoka Shabana mwanzoni mwa msimu huu, alidaiwa kushambuliwa na ndugu yake mdogo katika mzozo mkali kuhusu kipande cha ardhi ya familia.
Mchezaji huyo aliaga katika Hospitali ya Kaunti ya Kakamega alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































