KVF: KCB UGANI DHIDI YA SPIKERS
Kivumbi kinatarajiwa kutifuliwa katika ligi ya voliboli nchini, KVF, mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, KCB, watakapopambana na Young Spikers hii leo katika mechi ya mkondo wa pili ugani Kasarani Sports Centre Indoor Arena.
Wanabenki hao, chini ya uongozi wa Japheth Munala, watalenga kuvuna ushindi muhimu ili kupanda katika nafasi muhimu ya jedwali.
Kwa sasa wanashikilia nafasi ya 6 wakiwa na pointi 4, baada ya ushindi mmoja na kichapo mara 2.
Akizungumza kabla ya pambano hilo lililosubiriwa kwa hamu kubwa, Munala amekiri kuhusu uzito wa mechi hiyo, ila akatoa hakikisho kwamba wamejipanga sawasawa kuandikisha ushindi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































