VUGUVUGU LA UPINZANI PWANI LAMPIGIA DEBE KALONZO 2027
Vuguvugu linalounga mkono upinzani katika eneo la Pwani limemtaja kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka, kuwa mgombea anayefaa kupeperusha bendera ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Wakizungumza katika eneo la Tononoka, Mombasa, viongozi hao wamedai kuwa Rais William Ruto hajatekeleza ahadi alizotoa kwa wakazi wa Pwani, ikiwemo ajira kwa vijana, utatuzi wa migogoro ya ardhi na usambazaji wa rasilimali.
Aidha, wamedai kuwa ufisadi umechangia kuzorota kwa huduma muhimu kwa wananchi wengi, wakisisitiza haja ya mabadiliko ya uongozi kuelekea uchaguzi wa 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































