#Local News

KNH YATOA NOTISI KUHUSU MIILI ISIYODAIWA

Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta imetoa tangazo kwa umma ikizitaka familia kudai miili 480 iliyopo katika hifadhi yake, ikionya kuwa itazikwa ndani ya siku saba iwapo haitatambuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa hii leo, miili hiyo inajumuisha watu wazima 102 na watoto 378, jambo linaloonyesha uzito wa hali hiyo.

Uongozi wa hospitali hiyo umetoa wito kwa jamaa na walezi kujitokeza haraka kutambua na kuchukua miili hiyo ili kuepusha hatua ya kuizika kwa mujibu wa sheria.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *