STARLETS YATAJA KIKOSI CHA MUDA, SERENGE AITWA
Kocha wa Harambee Starlets, Beldine Odemba, ametaja kikosi cha muda cha wachezaji 31 kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya wanawake yatakayofanyika Nairobi kuanzia Aprili 11 hadi 15, 2026.
Kenya itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo yatakayofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo, yakishirikisha mataifa ya Australia, India na Malawi, huku wachezaji wakitarajiwa kuripoti kambini Aprili mosi.
Miongoni mwa walioteuliwa ni Marion Serenge anayepata nafasi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa, pamoja na kurejea kwa Terry Engesha na Mercy Airo kufuatia kiwango kizuri katika vilabu vyao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































