PASAKA: POLISI WAIMARISHA DORIA
Idara ya polisi nchini imetangaza kuimarisha doria na utekelezaji kikamilifu wa sheria za trafiki ili kuimarisha usalama kuelekea siku kuu ya Pasaka inayoanza Ijumaa hii.
Kupitia taarifa, inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, amesema hatua hiyo ni kutokana na safari nyingi, mikusanyiko pamoja na mvua kubwa ambayo huenda ikaendelea kuneysha wakati wa siku kuu hiyo.
Kulingana na taarifa hiyo, changamoto zaidi za kiusalama zimechangiwa na ujio wa Pasaka sambamba na kufungwa kwa shule kwa muhula wa kwanza, hivyo haja kwa maafisa zaidi kutumwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































