UDA PWANI YAKATAA MPANGO WA KUTENGA MAENEO
Viongozi wa chama cha UDA kutoka ukanda wa pwani wamepinga hoja ya kutenga maeneo na nyadhifa katika uchaguzi mkuu ujao.
Wakizungumza mjini Mombasa, viongozi hao wamesema watahakikisha vyama vyao na ODM vinashindana katika nyadhifa zote za pwani, wakipuuzilia mbali madai kuwa ODM kinaungwa mkono zaidi katika eneo hilo.
Aidha, viongozi hao akiwemo Spika wa Seneti Amason Kingi na katibu wa chama cha UDA Hassan Omar wamesema ODM haipaswi kuweka masharti kwa Rais William Ruto, wakisisitiza kuwa ushirikiano wa sasa unalenga kuhakikisha anapata muhula wa pili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































