MAENEO 59 TANA HATARI KUTOKANA NA MAFURIKO
Jumla ya watu 18 wamefariki kutokana na mafuriko katika siku za hivi karibuni baada ya watu 3 zaidi kufariki, serikali ikisema watu wengine 63 hawajulikani waliko huku wengine zaidi ya 60,000 wakiachwa bila makao.
Kulingana na takwimu za serikali, vifo hivyo vimeripotiwa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki, Kati, Bonde la Ufa, Nairobi na pwani huku serikali ikiwaagiza wakazi katika maeneo 59 katika eneo la Tana yaliyo karibu na bwawa la Seven Folks kuhama.
Wakazi wameitaka serikali kuwapa eneo mbadala.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































