UHURU ALENGWA KUPOKONYWA MANUFAA
Mswada wa kumpkonya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta marupurupu yake umeratibiwa kuwasilishwa leo katika bunge la seneti, Kenyatta akituhumiwa kuendelea kujihusisha na siasa licha ya kustaafu.
Mswada huo umefadhiliwa na seneta wa Nandi Samson Cherargei, anayesisitiza kuwa ni ukiukaji wa sheria kwa Kenyatta kuendelea kuikosoa serikali, hatua hii ikijiri baada ya rais huyo wa zamani kuishutumu serikali kwa madai ya kulenga kumnyima haki ya kujieleza kisiasa.
Hata hivyo, chama cha Jubilee kimepinga mswada huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































