MUSYOKA: KENYA INAVUNA UGOMVI WA FRANCOPHONE
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amepuzilia mbali dhana kwamba Kenya ni kitovu cha kibiashara barani Afrika kutokana na kuteuliwa kwa taifa hilo kuwa mwenyeji wa kongamano la Africa Forward Summit, akisema Kenya inajinufaisha na misukosuko inayoyakabili mataifa ya bara Afrika ambayo huzungumza lugha ya Kifaransa maarufu kama Francophone.
Kalonzo amemtaka Rais William Ruto kutoshabikia kongamano hilo, akisema licha ya Kenya kutazamiwa kuwa taifa lenya amani, bado linakaliwa na changamoto za ukiukaji wa haki za kidemokrasia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































