RASHFORD AWAPA BARCA UBINGWA LA LIGA
Bao la ikabu la Marcus Rashford liliwawezesha Barcelona kuwalaza mahasimu wao Real Madrid kwa kichapo cha mabao 2-0 katika mechi ya La Liga na kutawazwa mabingwa zikiwa zimesalia mechi 3 kabla ya ligi hiyo kutamatika.
Mshambulizi huyo wa Uingereza aliwaweka Barcelona kifua mbele kabla ya Ferran Torres kufunga la pili kuwapa miamba hao ushindi katika debi ya El Classico ugani Nou Camp.
Kwa sasa Barca wako mataji 7 nyuma ya Real ambao wanashikilia ubingwa huo mara nyingi, ila Barca wameshinda taji hilo kwa misimu miwili mtawalia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































