IEBC YACHACHISHA MAANDALIZI YA CHAGUZI NDOGO
Maandalizi ya chaguzi ndogo katika eneo bunge la Emurua Dikiir na uwakilishi wadi katika wadi mbili za kaunti ya Elgeyo Marakwet na Samburu yameshika kasi huku zikisalia siku mbili kabla ya chaguzi hizo kuandaliwa.
Tayari tume huru ya uhaguzi na mipaka, IEBC, imepokea masanduku yenye karatasi za kupigia kura, kabla ya chaguzi hizo za Alhamisi hii.
Vifaa hivyo vitaanza kusambazwa hii leo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































