MATHARE UNITED YATANGAZA KUONDOKA KWA KOCHA JOHN KAMAU
Mathare United imetangaza kuondoka kwa kocha mkuu John Kamau huku mechi tatu pekee zikisalia kabla ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya FKF 2025/2026.
Klabu hiyo imesema Kamau ataondoka mara moja kutoka nafasi yake ya ukocha huku Kocha msaidizi Mohammed Mchulla akipewa jukumu la kuiongoza timu hiyo kwa muda katika mechi zilizobaki za msimu huu.
Hatua hiyo imefuatia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya APS Bomet, matokeo yaliyoripotiwa kuwa sababu kuu ya uamuzi huo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































