GACHAGUA AIBUA MADAI YA UFISADI KWENYE ZIARA YA MACRON
Ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini imeendelea kuibua hisia mseto, kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua akiibua madai kwamba ziara hiyo ilihusu mashauriano kuhusu malipo ya shilingi bilioni 7 kwa mashirika ya Ufaransa baada ya kandarasi zao za kujenga barabara kufutiliwa mbali.
Kulingana na Gachagua, mashirika hayo yalipewa kandarasi ya kukarabati barabara ya Rironi- Mau Summit na serikali iliyopita ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, ila ikafutiliwa mbali na Rais William Ruto na kupewa mashirika ya Kichina.
Anadai kuwa lengo la kufutiliwa mbali kwa kandarasi hizo lilikuwa kufuja fedha za umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































