#Athletics #Sports

OMANYALA BADO ANA NJAA YA MAFANIKIO ZAIDI

Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala amesema bado hajaridhishwa na mwanzo wake mzuri wa msimu wa mwaka 2026 huku akilenga mafanikio makubwa zaidi.

Omanyala ameonyesha kiwango bora katika mashindano ya Diamond League nchini China ambapo aliibuka mshindi katika mbio za mita 100 kwa muda wa sekunde 9.94 mjini Xiamen.

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 30 aliwashinda Gift Leotlela wa Afrika Kusini pamoja na Trayvon Bromell wa Marekani, huku akiendelea kuthibitisha ubora wake duniani katika mbio za mita 100.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *