FEDHA ZITOKAZO UGHAIBUNI ZAPUNGUA KWA ASILIMIA 4.7
Fedha zinazotumwa nchini na Wakenya wanaoishi ughaibuni zilipungua kwa asilimia 4.7 mwezi Juni mwaka huu, kwa mujibu wa taarifa ya hivi punde ya Benki Kuu ya Kenya (CBK).
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa fedha hizo zilifikia takriban shilingi bilioni 48 mwezi Juni, zikishuka kutoka shilingi bilioni 50 zilizorekodiwa mwezi Mei.
CBK imesema kupungua huko kulichangiwa na kupungua kwa fedha zilizotumwa kutoka katika masoko makuu yanayokotoka fedha hizo. Hata hivyo, benki hiyo imesisitiza kuwa fedha zinazotumwa na Wakenya wa ughaibuni zinaendelea kuwa chanzo muhimu cha mapato ya fedha za kigeni nchini.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































