KENYA PIPELINE YATWAA UBINGWA WA KENYA CUP
Kenya Pipeline imetawazwa mabingwa wa Kenya Cup kwa upande wa wanawake baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3-2 dhidi ya wapinzzani wao KCB katika fainali ya kusisimua iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kasarani Indoor Arena.
Baada ya kupoteza seti ya kwanza kwa alama 25-21, Pipeline ilijibu kwa kushinda seti ya pili 25-12 na ya tatu 25-21. KCB ilirejea na kutwaa seti ya nne 25-23, lakini Pipeline ikashinda seti ya mwisho 15-11 na kutwaa ubingwa.
Ushindi huo umeiwezesha Kenya Pipeline kukamilisha msimu kwa kutwaa mataji mawili ya ndani ya nchi, baada ya pia kushinda ubingwa wa Ligi ya Taifa mapema msimu huu. Pipeline ilifika fainali kwa kuiondoa DCI, huku KCB ikifuzu baada ya kuwashinda Kenya Prisons.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































