#Local News

MGOMO WA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WASITISHWA

Ni afueni kwa wasafiri wanaotumia ndege baada ya Wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kusitisha mgomo uliokuwa umepangwa baada ya kusaini makubaliano ya awali na waajiri katika sekta hiyo.

Makubaliano hayo yanakuja siku chache baada ya Muungano wa KAWU kutangaza mgomo huku pande zote zikikubaliana kuanza mazungumzo kuhusu masuala ambayo bado hayajapatiwa suluhu.

Mazungumzo hayo yatalenga kushughulikia malipo ya mishahara, usalama wa ajira na kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *