SEREM AILETEA KENYA DHAHABU YA KWANZA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA
Edmund Serem ameiletea Kenya medali yake ya kwanza ya dhahabu katika Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 baada ya kushinda mbio za kuruka viunzi na maji za mita 3,000 mjini Glasgow, nchini Scotland.
Serem alimaliza mbio hizo kwa muda wa dakika 8:18.23, akifuatiwa na Simon Koech, aliyeshinda medali ya fedha kwa muda wa dakika 8:18.59, huku Leonard Bett akitwaa medali ya shaba kwa muda wa dakika 8:21.63.
Kenya ilitawala mbio hizo kwa kutwaa nafasi zote tatu za kwanza, na hivyo kuandika historia ya ushindi kamili katika fainali ya mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































