#Local News

KENNEDY KALOMBOTOLE AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mwanamume anayekabiliwa na mashtaka ya kumuua mgonjwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta Kennedy Kalombotole amefikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la mauaji baada ya kucheleweshwa kwa kesi yake kwa miezi kadhaa

Kalombotole alifikishwa mbele ya Jaji Diana Kavedza katika Mahakama Kuu jijini Nairobi ambapo alikana shtaka la mauaji.

Kesi hiyo ilikuwa imesubiri kukamilika kwa uchunguzi wa kubaini iwapo alikuwa na uwezo wa kiakili wa kujibu mashtaka yanayomkabili.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *