#Local News

SABINA CHEGE ATETEA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YA MATOKEO YA UCHAGUZI

Mjadala umezuka baada ya Tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC kutoa pendekezo la kusitisha zoezi kuwasilisha matokeo ya uchaguzi ya moja kwa moja.

Mbunge Mteule Sabina Chege amesema IEBC haijatoa sababu za kuridhisha za kusitisha matangazo au matokeo ya moja kwa moja ya matokeo ya uchaguzi.

Sabina Chege amesema zoezi hilo huwafahamisha Wakenya kuhusu mwenendo wa uchaguzi, huimarisha uwazi na husaidia kupunguza taharuki badala ya kuzua sintofahamu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *