#Local News

RUTO AWATAKA WAKENYA KUUNGANA KABLA YA 2027

Rais William Ruto amewataka Wakenya kudumisha umoja na mshikamano licha ya tofauti za kisiasa, huku taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2027.

Akizungumza nchini Zambia wakati wa kuapishwa kwa Rais Hakainde Hichilema kwa muhula wa pili, Ruto amesema ushindani wa kisiasa haupaswi kugeuka chanzo cha migawanyiko na migogoro nchini.

Amesisitiza kuwa uchaguzi unapaswa kuwa mashindano ya uongozi na si vita kati ya wananchi, akisema mambo yanayowaunganisha Wakenya lazima yazidi yale yanayowatenganisha.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *