#Local News

MGOMO WA WAUGUZI WAENDELEA LICHA YA MAZUNGUMZO NA MAGAVANA

Muungano wa Kitaifa wa Wauguzi na Wakunga unasema mazungumzo na Baraza la Magavana yanaendelea, lakini mgomo bado upo baada ya pande hizo kushindwa kufikia mwafaka.

Katibu Mkuu Seth Panyako anasisitiza kutekelezwa kwa Mkataba wa Makubaliano wa mwaka 2017, huku magavana wakipinga wakisema ulifikiwa chini ya shinikizo na hauwezi kutekelezwa.

Mvutano huo unaendelea hata baada ya Naibu Rais Kithure Kindiki kuagiza Wizara ya Afya kuwakutanisha wauguzi na magavana, ili kutafuta suluhu ya mgomo unaoathiri huduma za afya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *