FKF YAKUTANA NA VILABU KUTATUA MVUTANO WA LIGI
Shirikisho la Soka nchini FKF linakutana na viongozi wa vilabu Jumatano asubuhi katika juhudi mpya za kutatua mzozo wa kanuni na uongozi uliosababisha msimu wa 2026/27 wa Ligi ya SportPesa kusimama.
FKF inalenga kufikia mwafaka kuhusu mfumo wa kupandishwa na kushushwa daraja pamoja na kanuni zitakazotumika msimu huu, baada ya mkutano uliopangwa Jumatatu kuahirishwa kufuatia mashauriano na vilabu.
Mazungumzo hayo yanafanyika huku Mahakama Kuu ya Milimani ikiendelea kuzuia kuanza kwa ligi hadi kesi hiyo itakaposikilizwa Septemba 21, huku Rais wa FKF Hussein Mohammed akikiri maandalizi ya msimu yalifanywa kwa haraka na kusisitiza umuhimu wa mashauriano Zaidi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































