#Local News

SHILINGI 10  YA UGALI YAZUA VURUGU KAKAMEGA.

Mzozo wa shilingi kumi umeishia kwa vurugu mjini Kakamega baada ya mmiliki wa hoteli kupigwa mawe kufuatia mvutano na mteja wake.

Mzozo huo ulianza baada ya mteja kupinga kukatwa kwa shilingi kumi katika malipo yake ya ugali, hali iliyozua mabishano makali kati yake na mmiliki wa hoteli.

Tukio hilo liliibua vurugu huku mmiliki huyo akijeruhiwa baada ya kupigwa mawe na mteja huyo ambaye anasakwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *