BABU AONYA UPINZANI KUCHELEWA KUTEUA MGOMBEA WA URAIS
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameonya viongozi wa upinzani dhidi ya kuchelewesha uteuzi wa mgombea wao wa urais, akisema hatua hiyo inaweza kuzidisha mpasuko na kudhoofisha umoja wao kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Akizungumza jijini Nairobi, Babu amepinga pendekezo la kusubiri hadi Desemba 2026 kuanza mazungumzo ya kumteua mgombea mmoja, akisema wakati huo wanasiasa watakuwa wamejikita zaidi katika kulinda maslahi ya viti wanavyolenga.
Babu amesema upinzani unapaswa kufikia uamuzi mapema ili kumpa mgombea wa pamoja muda wa kutosha kufanya kampeni nchini na kujenga uungwaji mkono kabla ya uchaguzi wa 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































