MUDAVADI AFAFANUA AGIZO LA RUTO KUHUSU BIASHARA ZA WAGENI
Mkuu wa Mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi amesema agizo la Rais William Ruto kuhusu wageni wanaoendesha biashara ndogo zisizo rasmi lililenga kulinda sekta zilizo hatarini, kuhakikisha ushindani wa haki na kuhifadhi ajira na riziki za Wakenya.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje, agizo hilo halikulenga kuwapiga marufuku wageni wote kufanya biashara ndogo nchini, bali kuweka mazingira yenye utaratibu na yanayodhibitiwa kwa mujibu wa sheria.
Mudavadi amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha biashara ndogo zinaendeshwa kwa usawa huku maslahi ya wafanyabiashara na wananchi wa Kenya yakilindwa bila kuvuruga shughuli halali za kiuchumi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































