#Football #Sports

MAN UNITED YADHALILISHA SABAH 4-0

Kocha wa Manchester United Michael Carrick amesema tayari anaona mabadiliko katika uchezaji wa timu hiyo ikilinganishwa na msimu uliopita, baada ya kuanza kwa kishindo kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya

United iliichapa Sabah mabao 4-0 katika Uwanja wa Old Trafford kupitia mabao ya Matheus Cunha, Bruno Fernandes, Benjamin Šeško na Lisandro Martinez, katika ushindi uliowapa mwanzo mzuri kwenye mashindano hayo

Hata hivyo Carrick amesema matokeo hayo hayakuakisi ugumu wa mchezo, akifurahishwa na namna wachezaji wake walivyoweza kujenga mashambulizi katika maeneo yenye msongamano wa kiungo, jambo analolenga kulifanya kuwa sehemu ya mtindo wao wa uchezaji.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *