WACHIMBAJI MADINI WAWILI WAFARIKI RACHUONYO KAUNTI YA HOMABAY
Wachimbaji madini wawili wamefariki baada ya shimo la machimbo ya dhahabu kuwaangukia katika eneo la Kowidi Rachuonyo Kusini Homa Bay.
Tukio hilo lilitokea Jumatano, Septemba 9 wakati kuta za shimo hilo zilipoanguka na kuwafunika wachimbaji hao.
Waathiriwa, Samwel Omondi mwenye umri wa miaka 35 na James Raila, walikimbizwa Hospitali ya Kaunti ya Rachuonyo, lakini walifariki kutokana na majeraha.
Imetayarishwa na cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































