NAIBU RAIS RIGATHI GACHAGUA AHUDHURIA IBAADA YA WAFU YA WAADHIRIWA WA MAFURIKO MAIMAHIU

Rais Rigathi Gachagua, gavana wa nakuru Susan Kihika , mbunge wa naivasha Jane Kihara na viongozi wengine walihudhuria ibaada ya wafu ya watu 61 walioaga dunia kutokana na mafuriko eneo la maimahiu kaunti ya Nakuru.
Mkasa huo ulitokea tarehe 29 mwezi wa aprili ambapo bwawa la old Kijabe lilivunja kingo zake na kusababisha mafuriko eneo hilo.
Kanisa limeiomba serikali kuhakikisha waadhiriwa wanafidiwa kikamilifu ili kuwawezesha kuendelea na Maisha yao hata baada ya mkasa.
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































