#Local News

MAHAKAMA YASITISHA UTEUZI WA ZABLON MOKUA

Mahakama kuu imesitisha uteuzi wa Zablon Muruka Mokua kama jaji wa mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu haki kufuatia kesi iliyowasilishwa na chama cha waansheria nchini LSK wakisema hafuzu kuhudumu katika wadhifa huo.

Jaji wa mahakama hiyo Chacha Mwita, ametoa amri ya kuzuia kuidhinishwa kwa Mokua hadi kesi dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Mokua ambaye awali alihudumu kama mwakilishi wa wadi, aliteuliwa na Waziri peninah malonza mwezi Aprili, kuchukua nafasi yake Jaji Charles Nyachae aliyejiuzulu mapema mwaka huu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *