MUSYOKA: MNATUIBIA KUPITIA BAJETI
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ameshutumu makadirio ya jeti ya mwaka 2024-2025 yaliyowasilishwa hapo jana na waziri wa fedha Njuguna Ndung’u, akitaja mianya ya ufujaji wa fedha za umma.
Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, Kalonzo akiwaongoza viongozi wa Azimio amesema serikali inalenga kufuja kima cha shilingi trilioni moja kupitia mgao wa bajeti hiyo.
Aidha, Musyoka ameshutumu mapendekezo ya juu ya ushuru yanayopndekezwa kwenye makadirio hayo, akisema yatalemaza shughuli za biashara.
Imetayarishwa na Antony nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































