KENYA KUANGAZIA UPYA SERA YA MAMBO YA NJE ILI KUENDANA NA MWELEKEO WA DUNIA
Serikali kuu hapo jana imetoa wito wa kuangazia upya sera ya mambo ya nje ya nchi ili kuleta umuhimu na ufanisi katika kuhimiza maslahi na maadili ya kitaifa.
Waziri wa mambo ya nje ya nchi na diaspora Musalia Mudavadi amesema, mwelekeo wa dunia unaathiri ufanisi wa nchi na kufafanua upya sera ya mambo ya nje ya Kenya, hivyo mwelekeo huo lazima uangaziwe kwenye waraka wa Sera ya mambo ya mwaka wa 2024.
Aidha mudavadi ameongeza kuwa ni lazima kuendelea kutathmini na kurekebisha sera ya mambo ya nje ya nchi, ili kuhakikisha inaendelea kuwa muhimu na kuwa na ufanisi katika kuhimiza maslahi na maadili ya kitaifa.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































