TUTAUNDA CHAMA UPYA (UDA); HASSAN OMAR ASEMA
Katibu mkuu wa chama cha UDA hassan Omar anasema kuwa uongozi wa chama hicho una nia ya kurekebisha chama kufuatia mivutano iliyoshuhudiwa wakati wa kumtimua aliyekuwa katibu mkuu wa UDA Cleophus Malala.
Kwa mujibu wa Omar mipango ya kufanyisha uchaguzi wa mashinani katika maeneo ambako uchaguzi uliahirishwa ingali inaendelea ili kuhakikisha viongozi wapya wanachukua hatamu za uongozi kukiwa na nia ya kuungana na viama vingi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































