MARCO REUS AINGIA LA GALAXY
Kiungo wa zamani wa Borussia Dortmund na Ujerumani Marco Reus amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu kuichezea LA Galaxy, timu ya Ligi Kuu ya Soka nchini marekani.
Reus, 35, alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita, akicheza mchezo wake wa mwisho katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.
Iliondoa pazia katika kipindi cha miaka 12 katika klabu hiyo ya Ujerumani, ambapo alicheza michezo 429 katika mashindano yote na kufunga mabao 170.
Pia alicheza mechi 48 za Ujerumani na kushiriki Euro 2012 na Kombe la Dunia la 2018.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































