SIGEI ALAANI VURUGU KATIKA MIKUTANO YA KISIASA
Seneta wa Bomet Hillary Sigei amelaani vurugu na ukosefu wa uvumilivu katika mikutano na mikusanyiko ya kisiasa, akisema vitendo hivyo vinapaswa kukataliwa na kila Mkenya.
Sigei amesema hata wale ambao hawaungi mkono vyama vinavyohusika wanapaswa kulaani vurugu, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za kisiasa za wengine.
Kauli hiyo inajiri huku Kenya ikielekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, ambapo Sigei ametoa wito wa siasa za amani na uvumilivu ili kulinda mshikamano wa taifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































