#Football #Sports

GOR MAHIA YATOLEWA LIGI YA MABINGWA KWA KICHAPO CHA 5-1

Gor Mahia imeaga Ligi ya Mabingwa Afrika kwa fedheha baada ya kuchapwa mabao 5-1 na Pyramids FC ya Misri katika mchezo wa marudiano mjini Cairo na kutolewa kwa jumla ya mabao 7-1.

Pyramids ilifunga mabao matatu kipindi cha kwanza kupitia Walid El Karti, Nasser Maher na Yusuf Obama, kabla David Okoth kuifungia Gor Mahia bao la kufutia machozi dakika za mwisho za kipindi hicho.

Hata hivyo Pyramids iliongeza mabao mawili dakika za 90 na 91 kupitia Mustafa Ziko na Mahmoud Zalaka, huku kichapo hicho kikifunga safari ya K’Ogalo baada ya pia kupoteza mchezo wa kwanza Nairobi mabao 2-0.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *