#Local News

RUTO AJITETEA BAADA YA MIAKA MINNE MADARAKANI

Rais William Ruto amesema serikali yake imetimiza sehemu kubwa ya ahadi ilizotoa kwa Wakenya tangu ilipoingia madarakani miaka minne iliyopita, akipinga madai ya usimamizi mbaya wa uchumi na ufisadi.

Akizungumza katika ibada ya kanisa Kaunti ya Kisumu, siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano katika eneo la Nyanza, Ruto amesema serikali yake imepiga hatua katika kutekeleza ajenda yake ya maendeleo.

Rais pia amemsifu aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, akisema urithi wake wa kisiasa na mchango wake bado unaendelea kuathiri mwelekeo wa taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *