NPS IMEANZA KUTAMBUA MAENEO YANAYOWEZA KUKUMBWA NA GHASIA IFIKIAPO UCHAGUZI MKUU
Huduma ya Polisi nchini, NPS, imeanza kutambua maeneo yanayoweza kukumbwa na ghasia za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Gilbert Masengeli, amesema polisi watatumia taarifa za kiujasusi kutambua maeneo hayo na kuweka mikakati ya kuzuia vurugu.
Masengeli amesema polisi watahakikisha usalama wa wananchi unalindwa, huku akionya kuwa ghasia za kisiasa zinazochochewa na watu au makundi hazitakubaliwa nchini.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































