WAKAAZI WA RUAI WANAITAKA SERIKALI KUIMARISHA USALAMA ENEO LA MAPOROMOKO YA MAJI
Wakazi wa Ruai wameitaka serikali kuimarisha usalama katika eneo la maporomoko ya maji ya Ruai kufuatia vifo kadhaa vilivyoripotiwa katika eneo hilo.
Wakazi wamesema hali hiyo imezua hofu na wanahitaji hatua za haraka kuhakikisha usalama wa wanaotembelea eneo hilo.
Wameitaka serikali kuchunguza chanzo cha vifo hivyo na kuweka mikakati ya kuzuia matukio zaidi.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































