#Rugby #Sports

KCB YATETEKA UBINGWA WA SEVENS KWA MARA YA TATU

KCB RFC imetetea ubingwa wa Mzunguko wa Kitaifa wa Raga ya Wachezaji Saba kwa msimu wa tatu mfululizo licha ya kushindwa kufika fainali ya Christie Sevens jijini Nairobi.

KCB na mpinzani wake wa karibu Kabras Sugar walitolewa katika hatua ya nusu fainali kwenye Uwanja wa RFUEA Grounds, matokeo yaliyomaliza mbio za kuwania ubingwa wa msimu huo huku KCB ikitwaa taji kwa jumla.

Menengai Oilers kwa upande wao walitwaa taji lao la kwanza msimu huu baada ya kuichapa Strathmore Leos 24-12 katika fainali, huku KCB ikimaliza siku kwa kuifunga Kabras Sugar 5-0 katika muda wa ziada kupitia jaribio la George Ooro.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *