#Local News

RAIS ANAENDELEA NA ZIARA YAKE YA SIKU NNE NYANZA

Rais William Ruto ameendelea na ziara yake ya siku nne katika eneo la Nyanza, ambapo amefika Kisumu na kuzindua mradi wa maji na usafi wa mazingira wa Ziwa Victoria.

Akizungumza na wananchi wa Nyamasaria, Rais Ruto ametetea mpango wa serikali wa nyumba za bei nafuu,amesema Kisumu imetengewa shilingi bilioni 44 kwa ujenzi wa nyumba elfu 12, masoko 20 na mabweni elfu 12.

Rais Ruto amesema serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika eneo la Nyanza na kuhakikisha eneo hilo haliachwi nyuma.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *