LOTEE: KINDIKI HANA SABABU YA KUHOFIA NAFASI YAKE
Huku mjadala kuhusu nafasi ya Naibu Rais ukizidi kushika kasi, baadhi ya viongozi wanaendelea kupuuzilia mbali madai kwamba kuna mabadiliko yanayotarajiwa katika uongozi wa serikali.
Mbunge wa Kacheliba Titus Lotee amesema ODM haiwezi kumteua Naibu Rais, akieleza kuwa mamlaka ya kumteua mshikilia wadhifa huo yapo mikononi mwa Rais William Ruto pekee kwa mujibu wa Katiba.
Lotee amesema tamko la Junet Mohamed la kumtambulisha Wycliffe Oparanya kama Naibu Rais ni sehemu ya siasa za ushindani na halimaanishi kuwa Naibu Rais Kithure Kindiki yuko katika hatari ya kupoteza nafasi yake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































