#Local News

GITONGA: WIMBI LA SIFUNA LINAZIDI KUSHIKA KASI

Mwelekeo wa siasa za upinzani unaendelea kubadilika huku viongozi mbalimbali wakianza kutathmini ushawishi wa viongozi wanaojitokeza na vuguvugu jipya linalozidi kuvutia wananchi.

Mwaniaji wa kiti cha eneo bunge la Othaya Antony Gitonga amesema Edwin Sifuna amekuwa sura mpya yenye mvuto na tishio kwa baadhi ya wanasiasa kutokana na kuongezeka kwa umaarufu wake.

Gitonga amesema vuguvugu la Linda Mwananchi linaendelea kuimarika na kusisitiza kuwa ni wazo ambalo haliwezi kupuuzwa katika siasa za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *