ARSENAL WAKARIBIA KUMSAJILI BRUNO GUIMARÃES
Harakati za Arsenal kuimarisha kikosi chao kabla ya kuanza kwa msimu mpya zinaendelea kushika kasi, huku klabu hiyo ikielekeza nguvu zake katika kuongeza ubora wa safu ya kiungo.
Arsenal wanakaribia kumsajili nahodha wa Newcastle United Bruno Guimarães, huku ripoti zikieleza kuwa kiungo huyo wa Brazil anatamani kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu England katika dirisha hili la usajili.
Guimarães ameichezea Newcastle United mechi 195 na kufunga mabao 31 tangu alipojiunga mwaka 2022, huku ripoti zikieleza kuwa Arsenal wana imani ya kukamilisha usajili huo licha ya mazungumzo kati ya klabu hizo mbili kuendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































