#Local News

OUNDO: SIFUNA AMERITHI NGUVU NA WAFUASI WA RAILA

Mbunge wa Funyula Wilberforce Oundo amesema Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amerithi nguvu na idadi ya wafuasi wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, akidai kuwa Linda Mwananchi sasa imechukua nafasi ya ODM.

Oundo amesema uchaguzi wa Uwanja wa Jacaranda haukuwa wa kawaida bali ulikuwa ishara ya kutangaza ushawishi wao jijini Nairobi, akisema mapokezi waliyopewa na wananchi yamewapa matumaini ya kushinda uchaguzi ujao.

Mbunge huyo pia amesema ODM imekufa kisiasa na kwamba Linda Mwananchi iko tayari kutawala, huku akieleza matumaini ya muungano huo kumuondoa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *