#Local News

MCHAMBUZI: ODM IMEPOTEZA NGUVU KISIASA NAIROBI

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Fwamba NC Fwamba amesema ODM ya sasa haina nguvu ilizokuwa nayo wakati wa aliyekuwa kiongozi wa chama hicho Raila Odinga.

Fwamba amesema kwa sasa ODM ina ushawishi mkubwa zaidi katika eneo la Nyanza, huku chama hicho kikionekana kupoteza nguvu ya kisiasa kilichokuwa nacho jijini Nairobi.

Amesema mabadiliko hayo yanaashiria kupungua kwa ushawishi wa ODM katika baadhi ya maeneo muhimu ya kisiasa, hasa ikilinganishwa na kipindi ambacho Raila Odinga alikuwa akiongoza chama hicho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *