HASSAN OMAR AJITETEA KUHUSU KAULI YA KURA ZA WAFU
Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar sasa amesema kauli yake kuhusu kura za wapiga kura waliofariki ilichukuliwa nje ya muktadha, akisema lengo lake lilikuwa kuwahamasisha Wakenya kujisajili na kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Omar amewashutumu viongozi wa upinzani kwa kupotosha matamshi yake na kupanga kuyatumia kudhalilisha chama tawala kwa manufaa ya kisiasa, akisisitiza kuwa hakulenga kuhalalisha matumizi ya kura za wafu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































