#Local News

LINDA MWANANCHI YAINGIA NAIROBI KWA MSAKO WA UMOJA WA UPINZANI

Viongozi wa Linda Mwananchi wamewasili jijini Nairobi huku maelfu ya wakazi wakijitokeza kuwaunga mkono katika msafara wao wa kisiasa uliolenga kuingia katikati ya mji.

Timu hiyo ilihutubia wafuasi katika vituo kadhaa kabla ya kuelekea uwanja wa kihistoria wa Jacaranda, huku viongozi wakisema wamedhamiria kuwasilisha mgombea mmoja wa urais wa upinzani atakayekabiliana na Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027.

Katika ishara ya kutafuta umoja, Gavana wa Siaya James Orengo amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kwa lengo la kupata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya Linda Mwananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *